Dalili 7 za Vidonda Vya Tumbo na Tiba
Leo Tumekuletea aina ya Dalili zinazosababisha Vidonda hivi Vya Tumbo na Tiba, Kwanza Tuangalie Aina ya Vidonda Vya Tumbo.
Aina Za Vidonda Vya Tumbo:
Vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni;
1) Vidonda Vya Tumbo Kubwa.
Hivi ni vidonda ambavyo tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa (stomach).
Vidonda hivi vya tumbo hujulikana kwa kitaalamu kama Gastric ulcers.
Peptic ulcers
2) Vidonda Vya Utumbo Mdogo.
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum.
Vidonda hivi vya tumbo hujulikana kwa kitaalamu kama Duodenal ulcers.
Duodenal ulcers
Sababu Za Vidonda Vya Tumbo:
Yafuatayo ni mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ambayo ni pamoja na;
1) Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori).
2) Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine).
3) Msongo wa mawazo.
4) Kula vyakula vinavyozalisha asidi kwa wingi.
5) Kunywa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.
6) Uvutaji wa sigara.
7) Kutokula mlo kwa mpangilio.
8) Kansa ya tumbo.
Hizi hapa Dalili Za Vidonda Vya Tumbo:
Zifuatazo ni dalili za vidonda vya tumbo ambazo ni pamoja na;
1) Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula.
2) Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo.
3) Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa.
4) Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu.
5) Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu.
6) Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.
7) Kushindwa kupumua vizuri.
Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo:
Tatizo la Vidonda hivi linatibika kufuatana na muda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.
Dawa za Asili: Inapendekezwa Kutumia Juice ya Kabeji, pia tumia Asali Mbichi ,kula Karoti, Tumia Unga Wa Majani ya Mlonge , kula Ndizi au meza Punje za Kitunguu Saumu.
Usile au punguza vyakula vyenye ACID au vilivyokaangwa kwa kiasi kingi cha mafuta kama chipsi na kuku wa kukaanga. Kula vyakula vyenye asili ya nafaka isiyo kobolewa mfano dona na vyakula vyenye kiwango kidogo cha mafuta pamoja na mboga za Majani.
Dawa zinazotolewa hospitali kwa ajili ya kutibu ni pamoja na;
a) Amoxicillin tabs.
b) Omeprazole tabs/pantoprazole tabs.
c) Metronidazole tabs (Flagyl).
Madhara Ya Vidonda Vya Tumbo:
Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa wa vidondahivi atashindwa kupata tiba mapema;
1) Kansa ya tumbo (Gastric cancer).
2) Kutoboka kwa kuta za tumbo (Gastro-intestinal perforation).
3) Kuvuja damu kwa kuta za tumbo (Gastro-intestinal bleeding).
4) Kutapika damu (hematemesis).
5) Upungufu wa damu (anaemia).
6) Kujisaidia kinyesi cheusi kama cha mbuzi (black orTarry stool).
7) Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (obstructed digestion).
Jinsi Ya Kujikinga Na Vidonda Vya Tumbo:
1) Jijengee tabia ya kunywa maji mengi kila siku.
2) Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguzia na mawazo.
3) Punguza (balansi) kiwango cha halemu (cholesterol).
4) Usivute sigara.
5) Punguza au acha kunywa pombe.
6) Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali.
7) Tenga muda wa kutosha wa kupumzika–unashauriwa kulala masaa 7 hadi 9 kila siku.