Njia 10 Jinsi ya kupata watoto mapacha

jinsi ya kupata watoto mapacha

Jinsi ya Kupata Watoto mapacha

Tati zinaonesha kwamba uwezekano wa mwanamke mmoja kubeba mimba ya mapacha ni 3%, na kuna njia mbalimbali zinaweza kuongeza uwezekano huu mpaka asilimia tano au 10.

Also You Can Read This: Jinsi ya Kuandika Barua ya kazi (Mifano)

Baadhi ya wanawake wanatamani kuwa na mapacha, lakini licha ya uzuri wa mapacha, wanawake wengine hawataki kabisa kusikia wakihoa pengine changamoto za kujifungua na malezi.

Aina mbili za Watoto Mapacha

1. Mapacha wa kufanana, ambao hutokea pale yai la mwanamke lililorutubishwa na na mbegu ya mwanaume
linapogawanyika na kutengeneza watoto wawili. Hawa hufanana sura, tabia, jinsia na mambo mengine na huwa vigumu sana kuwatofautisha.

2. Mapacha wasiofanana. Hawa hutokea pale mayai mawili ya mama yanavyorutubishwa na kujishikiza tofauti kwenye mfuko wa uzazi. Mapacha hawa hua wako tofauti kwa sura, jinsia na hata tabia.

Kupata Watoto mapacha

Je! Unawezaje kupata watoto mapacha?

Hakuna njia ya moja kwa moja ya kupata watoto mapacha lakini kuna baadhi ya mbinu zinazoongeza nafasi kubwa yakubeba mimba ya watoto mapacha ambazo ni pamoja na:

Njia 10 Jinsi ya kupata watoto mapacha

1. Chagua mpenzi wa aina hiyo;

Kama unatoka familia ambayo mapacha wanazaliwa mara kwa mara uko kwenye uwezekano mkubwa wa kuzaa mapacha nakama ukizaa na mtu ambaye kwao kuna mapacha wa mara kwa mara basi na wewe una nafasi kubwa ya kuzaa mapacha.

Hii ni njia ngumu kidogo kwani sio rahisi kujua utampenda nani maishani mwako.

2. Umri mkubwa

Mwanamke akifkisha umri wa miaka 35 na kuendelea kunatokea mabadiliko ya mfumo wake wa uzazi kiasi kwamba mwili wake huanza kuachia mayai mawili kila mwezi badala ya yai moja kama ilivyokawaida, na hii huongeza nafasi kubwa sana ya yeye kubeba mimba ya watoto mapacha.

3. Dawa za uzazi;

Kuna dawa ambazo hutumiwa na wanawake ambao wanashindwa kubeba mimba, dawa hizi hufanya yai zaidi ya moja kuachiwa kutoka kwenye mirija ya uzazi na hii huongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mapacha, na wanawake wanaotumia dawa hizi hujikuta wanabeba mapacha.

4. Kuwa na watoto

Wanawake ambao wamezaa mtoto mmoja au wawili kabla wana nafasi kubwa sana ya kuzaa mapacha kuliko wale ambao hawajawahi kuzaa kabisa. Ukifuatilia mapacha wengi hua hawazaliwi mimba ya kwanza ila kuanzia mimba ya pili kwenda mbele.

5. Kupata mimba ukiwa kwenye dawa za majira

Japokuwa sio rahisi sana lakini tati zinaonesha kwamba mimba zinazoingia kwa bahati mbaya mwanamke akiwa anatumia dawa za uzazi wa mpango hutengeneza mapacha lakini pia mimba zinazoingia muda mfupi baada ya kuacha dawa za uzazi wa mpango hua zinaleta watoto mapacha.

6. Urefu na unene

Tati zinzonesha kwamba wanawake warefu wana nafasi kubwa sana ya kubeba mimba za mapacha kuliko wanawake wafupi, lakini pia wanawake wanaobeba mimba wakiwa wanene wanakua na nafasi kubwa sana ya kupata mapacha.

7. Vyakula

Jamii ambazo chakula chao kikuu ni viazi vikuu, zimeonesha kuwa na mapacha wengi kuliko jamii zingine. Tati zinasema kwamba viazi hivyo vina kiasi kikubwa sana cha homoni za Oestrogen ambazo zinasababisha mama kutoa mayai mengi, kitaalamu kama Hyperovulation.

8. Nyonyesha mtoto kwa muda mrefu

Kuna homoni moja inaitwa prolactin ambayo inahusika na kutoa maziwa kipindi mama ananyonyesha, sasa kuendelea kuwepo kwa homoni hii kwa kiasi kikubwa wakati mama ameanza kushiriki tendo la ndoa kuna mwongezea nafasi kubwa ya kupata mapacha akibeba mimba.

9. Folic acid

Dawa za folic acid hutumika na wajawazito wote ili kuzuia uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo ya kimaumbile hasa kwenye mishipa ya fahamu, lakini matumizi ya dawa hizi mwezi mmoja kabla ya kubeba mimba yanaongeza uwezekano mkubwa wa kubeba mimba za mapacha.

10. Kuwa pacha mwenyewe

Hii najua inaweza isiwe kosa lako kama hukuzaliwa pacha, lakini kama wewe mwenyewe ulizaliwa kama mapacha basi uwezekano wa kubeba mimba ya mapacha ni mkubwa sana kuliko wale wengine ambao walizaliwa kawaida.

Hata hivyo, mwisho wa siku jambo kubwa ni kupata mtoto. Hivyo, ama ni mapacha au mmoja mmoja, wote ni watoto.