Mixes 6 Za Kusikiliza Wikendi Hii
Kwa watu na mashabiki wengi wa muziki Aprili ni mwezi wa shamra shamra na sherehe na kwa kulitambua hilo, tumekuandalia mixes 6 ambazo bila shaka zitakuburudisha na kuchangamsha wewe na na familia yako.
Subscribe ili kupata DJ Mixes zaidi hapa Mdundo: https://mdundo.ws/YingaM
Kuanzia kwenye muziki aina ya Qaswida mpaka kwenye Bongo Fleva hizi hapa ni mixes 6 kutoka ambazo unapaswa kusikiliza kwa wikendi hii:
Qaswida za Ramadhan Mix
Kama uko kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan basi mix hii mujarab yenye Qaswida za kushiba ikiwemo Thank You Allah, Inshaallah na Kurudha Za Ramadhani ni kwa ajili yako.
Ukiweka kando mawaidha mazuri utakayoyapata kwenye DJ Mix hii ya Ramadhan lakini pia itakupa hamasa zaidi ya kuswali na kufanya ibada.
Link: https://mdundo.com/song/2899951
New Bongo Fleva Xtra Affairs
Wasanii wote wanaofanya vizuri Bongo ikiwemo Platform, Nandy, Baddest 47, Kusah na Marioo utawakuta kwenye mix hii ambayo imesheheni ngoma kali za Bongo Flava ambazo bila shaka zitakosha mtima wako.
Humu ndani utapenda muingiliano wa sauti baina ya Platform na Ruby kwenye “Vitamu”, utafurahia sauti tamu ya Kusah kwenye “I Wish” pamoja na melody kali kutoka kwa Marioo kwenye “Wow”. Bila shaka hii sio mix ya kukosa.
Link: https://mdundo.com/song/2924969
Download Bongo Old School
Hakikisha hupitwi na Mix hii kali iliyokusanya ngoma za Bongo Fleva kutokea miaka ya nyuma.
Kuanzia hit song ya Professor Jay “Nikusaidiaje” kwenda kwenye ngoma ya Hussein Machozi ya “Kafia Ghetto” mpaka “Hasara Roho” ya Darassa, bila shaka hii ni mix ambayo imelenga kukusafirisha miaka kadhaa nyuma na kukupa kumbukumbu nzuri ya miaka ya nyuma.
Link: https://mdundo.com/song/2925760
Amapiano Latest Vibe Mp3 mix 2024
Haijalishi uko club, nyumbani au ume-chill na marafiki zako, hakikisha unasikiliza au kupakua mix hii kali ambayo ina ngoma za Amapiano kutoka Tanzania
Kwenye mix hii utakutana na sauti ya Jay Melody kwenye “Mapozi”, sauti ya Marioo na Tayla kwenye “Amawele” pamoja na chemistry poa baina ya Diamond na G Nako kwenye “Komando”. Kama unapebda ku-vibe na kufurahi mix hii ni ya kwako.
Link: https://mdundo.com/song/2924970
Download Latest 2024 Singeli Mp3 Mix
Unapenda muziki wa Singeli? Kama jibu ni ndio basi hakikisha unaipakua na kuisikiliza mix hii ambayo imekusanya Singeli zenye ubora wa TBS kutoka kwa wasanii nguli kama Mfalme Ninja, Meja Kunta na Balaa MC.
Sherehesha siku yako kwa kusikiliza mix hii ya Singeli yenye vibe la kutosha.
Link: https://mdundo.com/song/2925759
Bongo Flava Latest Mp3 Mix
Yetu matumaini umeshaisikiliza au kupakua mix hii ya kijanja yenye ngoma kali za Bongo Fleva kutoka kwa heavyweights tofauti tofauti kama Jay Melody, Jux, Tommy Flavour na Platform.
Ngoma nzuri za mapenzi zilizopo kwenye mix kama “Sugar Remix” “Juu” ya Genius Juu na “Simuachi” ya Jux bila shaka zitachangamsha siku yako.