Zifahamu Aina za Bima za Magari

zijue aina Bima za Magari

Bima za Magari Tanzania

CAIRO INTERTRADE COMPANY LIMITED – Washauri na Waagizaji Magari

Bima za Magari ni nini?

Ni mfumo wa kulipa kiasi kidogo cha pesa kwa kampuni ya bima ili kujilinda na madhara yanayoweza kujitokeza kwa siku zijazo.

RELATED: Subaru Forester Review | Bei yake | Engine | Tanzania

Kwa nini Bima kwenye gari yako?

  • Wajibu wa kisheria
  • Kujikinga dhidi ya hasara za ajali
  • Kujihakikishia usalam pindi usababishapo ajali

Hizi hapa Aina za Bima za Magari

1. Third Party. Mara nyingi huitwa Bima ndogo. Hukatwa kwa mujibu wa sheria kuwalinda watumiaji wengine wa barabara…Lugha nyepesi ni kwamba ukatapo bima hii unakua umewakatia watumiaji wengine wa barabara huku ukikiacha chombo chako na wewe mwenyewe bila bima

2. Third Party Fire & Theft. inafanya kazi kama hiyo ya kwanza, uzuri hii unakua umekikinga chombo chako na madhara ya moto pamoja na wizi wa vifaa au gari lote

3. Comprehensive. Maarufu kama bima kubwa hii inalinda watumiaji wa barabara, chombo chako na wewe mwenyewe kwenye madhara yatokanayo na ajali, moto au wizi

Bima ipi ni muhim kwa chombo changu?

Bima iitwayo comprehensive au mseto hii ni muhimu zaidi kuliko hizo nyingine kwa kua unakua umethamini chombo chako na wewe mwenyewe kwa kujikatia Bima hii kuliko hiyo third party unayokua umekatia watu au vitu vingine pekee

Napataje haki ya kulipwa bila usumbufu iwapo nina bima kubwa?

1. Hakikisha gari yako inapigwa picha pande zote, ndani, injini pamoja na chasis namba

2. Unatakiwa kuripoti tukio la ajali kwa kampuni husika bila kuzidisha masaa 24

3. Utatakiwa kuwasilisha form maalum ya polisi inayoelezea tukio husika

4. Ajali inatakiwa ithibitishwe haikua ya uzembe wako mfano hukua umetumia kilevi, hufanyi service ya gari kama kubadiri matairi n.k

5. Huruhusiwi kujitengenezea gari ndipo ukadai fidia

6. Iwapo unapata changamoto toka kampuni husika na haki iko upande wako, utatakiwa kuwasiliana na TIRA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bima) wakupatie msaada na ikishindikana unaweza kwenda mahakamani

7. Ajali za kutengeneza hazitolipwa na ikibainika unawezafikishwa mahakamani kwa uhujum uchumi

Mengineyo kuhusu Bima za Magari

1. Iwapo una third party au comprensive ukagonga gari ya mtu huwajibiki kumlipa kutoka mfukoni isipokua kampuni husika…uliyemgonga anatakiwa kupata taarifa zako za bima awasilishe kwenye kampuni husika na athibitishe kupitia maelezo ya polisi kwamba wewe ndio uliyegonga

2. Hakikisha chombo chako kipo kwenye mfumo wa serikali yaani TIRAMIS

Gharama

1. Third Party kwa magari madogo ni 118,000
2. Third Party Fire and Theft gari ndogo ni 177,000
3. Comprehensive gari ndogo itachajiwa asilimia 3.5 ya thamani ya gari jumla na VAT(18%)

Tumeona kushare nanyi ujumbe huu sababu furaha yetu ni kuona chombo ulichoagiza nasi kwa mamilioni kinaendelea kuwepo barabarani hata baada ya ajali baada ya wewe kupata fidia. usikatie watumiaji wengine chombo chako ukakikaacha.

Mawasiliano
+255 653 953 900 au tembelea ofisi zetu za Dar es Salaam,

Office Location: PSSSF HOUSE, 6th floor, Samora Avenue St -Dar es salaam.

#Bima za Magari # aina za Bima za Magari