Hisili Music
Ni bendi ya muziki wa asili kutoka Tanzania inayojulikana kwa kuchanganya miondoko ya hip hop na muziki wa asili. Bendi hii ilianzishwa mwaka 2023 mkoani Mbeya, katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
Asili ya Jina
Jina Hisili linatokana na muunganiko wa maneno mawili: Hip Hop na Asili, yakimaanisha mtindo wa muziki unaochanganya midundo ya kisasa na ala za kitamaduni za Kiafrika.
Mtindo wa Muziki na Ala
Hisili Music inatumia ala za muziki za asili ambazo hutengenezwa kienyeji, zikiwemo:
- Gitaa la nyuzi tatu
- Ngoma za jadi
- Babatoni (aina ya besi ya kitamaduni)
- Midundo ya banjo
Wasanii wa Band ya Hisili Music
Bendi ya hii inaundwa na wasanii wafuatao:
- Pius Polland – Mwandishi na mwimbaji
- Yusuph Shitindi – Mwimbaji na mpiga ngoma
- Mkapa Shiga – Mpiga gitaa la risasi na mwimbaji
- Yohana Mwalyego – Mpiga besi / babatoni
Muziki na Umaarufu
Mwaka 2025, Hisili Music walitoa EP yenye nyimbo tano iliyopewa jina Hisili Ngoma Yetu. EP hii inajumuisha nyimbo maarufu kama:
- Twende Pamoja (wakishirikiana na Wamwiduka Band)
- Salome
- Jana Na Leo
Hata hivyo, Hisili Music pia wamewahi kutoa nyimbo nyingine ambazo zilifanya vizuri kama Nasema na Wewe na Kipepeo, ambazo pia zimepokelewa vyema na mashabiki.
EP hii inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki ikiwemo Apple Music, ,YouTube, Boomplay na Audiomack.
Mwaka 2025, Â waliendelea kukuza muziki wao na kuimarisha uwepo wao kwenye majukwaa ya kidijitali.
Bendi hii imejizolea mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii, ikiwa na zaidi ya 100,000 wafuasi kwenye TikTok na zaidi ya 1,000,000 watazamaji kwenye YouTube.
Mchango kwa Jamii
Hisili Music inavutia sana mtaani kutokana na nyimbo zao zinazogusa hisia, kuelimisha jamii, na kuonyesha maelewano ya karibu pamoja na umaridadi wao katika muziki,
Wafuate Katika Mitandao yao ya Kijamii:
- TikTok (@hisili_music)
- YouTube ( Hisili Music )
- Instagram (@hisili_music)