Je Biashara ya Nafaka ni Nzuri? Jifunze Hapa

Biashara ya Nafaka

Biashara ya Nafaka

Moja ya Biashara nzuri kufanya, Hii sio biashara ya msimu, ni biashara ya mwaka mzima kutokana na uhitaji wake wa kila siku.
.
Anza kwa kuandaa mchanganuo mfupi wa biashara ya Duka la kuuza Mazao ya Nafaka.
.
Andika mahitaji yote ya muhimu unayotakiwa kuwa nayo ili kuanzisha biashara ya kuuza Nafaka na mazao ya kilimo mfano alizeti, soya, mahindi,Unga,Mchele, Sukari, karanga,mafuta ya kula pia Mizani ya kupimia , mifuko nk.

Mfanyabiashara: Usikose Hizi App Kwenye Simu Yako
.
Tambua umelenga kuwauzia wateja wa aina gani,Jumla au rejareja?
.
Eneo ulipo lina uhitaji mkubwa sana? kuna wakulima? Ukijua Itakusaidia kujua bei ya kuuza.
.
MTAJI.
Utahitaji mtaji fedha kununua
Nafaka pamoja na
gharama zingine zote kama kukodi eneo la Biashara, usafiri, nk.
..
Makadirio ya mtaji ni kuanzia 5M kwa mjini, lakini mtaji unaweza kupungua au kuongezeka kulingana na mahali.
.
Kabla ya kununua vitu ni muhimu kufanya tafiti ya bidhaa gani inahitajika usije kuleta maharage mengi kumbe eneo lako wanahitaji unga zaidi na wana mboga zao za majani, kwaio kipindi unaanza usiweke mtaji wote kwenye kununua nafaka acha kidogo ili ujue nini kinatoka zaidi na uongezee.
.
Tafuta ENEO lenye mzunguko mkubwa wa watu kama maeneo ya makazi, centre na kwenye masoko.
.
Nafaka utanunua kwa wakulima au kwa mawakala wakubwa wanaouza Mazao ya nafaka kwa bei ndogo. Tafuta connection mikoa ya wakulima ikiwezekana nenda
.
Kama huna mtaji mkubwa unaweza anza kwa kuongeza thamani nafaka, mfano kuweka kwenye package nzuri za kilo 1,2 5,10 na kuuza. Unaweza weka nembo yako pia.
.
Kama mtaji mkubwa unaweza safirisha kutoka mikoani kuja kuuza Dar es Salaam.
.
Biashara hii pia ni nzuri kwa waajiriwa kwani nafaka ni vitu vivyohesabika hivyo unaweza kufatilia mauzo ukiendelea na kazi.
..
Pia unaweza kuwa dalali wa mazao. (Tutajifunza siku nyingine hii)
.
Hii ni BIASHARA ambayo kwa vijana haijachangamkiwa sana na ukiangalia hakuna mtu ambaye amejenga Brand kubwa kwenye hii biashara kama Biashara nyingine hivyo kama una nguvu unaweza changamkia ukafanya kwa ukubwa.
.
Karibu, tujadili biashara hii kila mtu ajifunze, unaipenda, zipi changamoto na faida yake.

Pia Wengine Huuliza: Ninaomba kujuzwa , ni mazao aina gani naweza kuwa na soko zuri hapa mjini Dar? Na je ni mtaji kiasi gani naweza kuanzia nao? Natanguliza thanks.

Unaweza Kupata Majibu yake Hapa === Wafanyabiashara hapa.