Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi
Miaka ya zamani, tumbo kubwa lilihusishwa na utajiri, au uwepo wa mafanikio kwenye maisha. Mambo yamebadilika. Tumbo kubwa huondoa urembo kwa wanawake, au utanashati kwa wanaume.
RELATED: Vyakula Hatari Kwa Vidonda Vya Tumbo
Zifuatazo ni Njia 6 Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi.
1. Kunywa Maji Mengi
Kunywa maji mengi mara kwa mara kwa siku itakusaidia kuto kusikia njaa, Pia Jizoeshe Kunywa maji ya Moto kila Asubuhi Kabla Hujala Chochote Lita 1.
Pia Hii itakufanya uwe mbali na vyakula vyakula vya hapa na pale visivyo kuwa na msingi lakini pia maji yana saidia kufanya ngozi iwe nyororo
2. Punguza Au Acha Kunywa Soda
Sukari ni moja ya vitu vibaya vinavyo anzisha/kuleta unene kaa mbali nazo na anza kunywa maji kwa wingi
3. Weka Ratiba Ya Chakula
Ni vizuri kama utakuwa unajipikia mwenyewe maana utajua uweke chumvi, sukari kiasi gani, mafuta nk.
Pangilia ratiba yako ya week nzima lakini pia katika ratiba yako weka healthy food ambazo zitakufanya uweze kupuguza mafuta mwilini
4. Acha Kula Vitu Vidogo Vidogo
Biscuits, Big G, Chocolate ni vitamu na vina temptation sana lakini navyo vinaongeza sukari na kusababisha kuleta unene tumboni jaribu kuviepuka sana
5. Jitaidi Ule Taratibu
Hapa huwa tunashindwa sana, lakini kula taratibu kuna saidia kumeng’enya chakula chako vizuri lakini pia kunafanya ule chakula kidogo na kushiba haraka.
6. Epuka Vyakula Vya Mafuta
mafuta ni mabya sana katika chakula jaribu kutumia mafuta yenye less cholesterol, kama mafuta ya nazi, olive oil, almond au pika chukuchuku ukiongezea chakula chako na parachichi.
Parachichi linaweza kusababisha chakula kiwe kitamu na lina mafuta ambayo hayana madhara.
NB: Jitahidi Ufanye Mazoezi Angalau hata Dakika 15 kwa Siku hakikisha umetoka kijasho.
#Njia 6 Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi #Njia 6 Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi #Njia Rahisi Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi # Namna Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi #Njia 6 Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitam #Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi