Siku Za Hatari Na Siku Za Kushika Mimba

Siku Za Kushika Mimba

Siku Za Kushika Mimba

Kila mwanamke ana siku yake ambayo ni hatari zaidi kushika mimba. Siku hii inaweza kufanana na mwanamke mwingine ambaye anafanana naye mahesabu. Hata hivyo wanaweza kutofautiana kutokana na vyakula, maumbile na hali za maisha. Hapa nitakuletea orodha ya siku hatari za mwanamke.

Nini maana ya siku hatari?

Hizi ni siku ambazo mwanamke anakadiriwa kupata ujauzito. Ni mfululizo wa siku ambazo makadirio ya mwanamke kupata ujauzito ni mkubwa kuliko siku nyingine. Kabla ya kuzijuwa siku hizi kwanza hakikisha unajuwa vyema idadi ya siku mwanamke anazokwenda hedhi. Wanawake wanakwenda hedhi ndani ya mzunguruko unaoanzania siku 21 mpaka 35. hii inamaana kuna am,bao siku zao ni nyingi na wengine ni kidogo.

RELATED: Uhakika Njia 6 Jinsi Ya Kupunguza Tumbo au Kitambi

Sasa ni ipi siku hatari kwa mwanamke, siku ambayo mawanamke atapata ujauzito?. siku hii nitakuorodheshea, ila kwanza nataka tu nikujuze kwa ufupi sifa ya siku hiyo. Kwa nini, ni kwa sababu siku hizi zipo nyingi na zote ni hatari kwani zinaweza kuleta mimba. Ila katika hizo ipo ambayo ni hatari zaidi. Siku hiyo ina sifa hizi:-

1. Mwili wa mwanamke katika siku hii utakuwa na joto kulinganisha na siku zilizopita. Kwa urahisi unaweza kugunduwa kama unatumia kipima joto. Ila ukiwa makini unaweza kujigunduwa kama joto lako limepanda. Hakikisha ongezeko hiki ka joto hakiambatani na shida nyingine za kiafya kama maradhi.

2. Uteute unaopatikana kwenye shingo ya kizazi utakuwa umeongezeka na ni wenye kuteleza kama vile majimajiya yai lililopasuliwa. Kama utaingizakidole ndani zaidi ya uke unaweza kuupata kwenye kidole chako.

3. Siku hii hamu ya kushiriki tendo la ndoa nikubwa kuliko siku yingine. Hii haina haja ya kuielezea. Kama mwanamke homoni zake hazina shida basi lakima kutakuwa na siku ambayo atahitaji sana kushiriki ngono kuliko siku nyingine.

Nitaijuwaje siku hatari, ya kupata mimba?

Tazama Jedwari Hapa Chini

Mzunguko wa Mtu wa Siku 32

siku za kupata mimba

Mzunguko Wa Mtu Wa Siku 28 

siku za mimba

Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:–

1.  Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 – 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.

2. Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.

#Siku za Kupata Mimba #Hatari Siku Za Kushika Mimba  #Siku Za Kushika Mimba #Siku Za Kushika Mimba #Siku Za Kushika Mimba #Siku Za Kushika Mimba #Siku Za Kushika Mimba #Siku Za Kushika Mimba #dalili ya siku za hatari kwa mwanamke #siku ya mimba kuingia #siku za kupata mimba baada ya hedhi