Home Gospel Inasemekana Huu ni Mti Hatari Ukipanda Nyumbani Kwako

Inasemekana Huu ni Mti Hatari Ukipanda Nyumbani Kwako

Yale maingiliano ya dunia ya kiroho na dunia isiyoonekana huthibitishwa na matokeo yake na si mchakato unaoonekana Kwa wale ndugu zangu wanaotaka ithibati za kisayansi naomba watulie wasome kimyakimya tuu.

Kuna huu mti unaopendwa kupandwa kuzunguka nyumba zetu, ni mti mzuri wenye kivuli kizuri, hujulikana kama mti mwamvuli na matawi yake huota kwa mpangilio maalum na wengine huuita Mti wa Panga Uzazi.
Ni mti wenye mizizi mirefu yenye nguvu ya ajabu kiroho katika ulimwengu uonekanoa Mizizi yake yenye nguvu huweza kupenya kwenye msingi wa nyumba na kusababisha ufa au nyufa na kuleta uharibifu mkubwa kwenye jengo lako.

Nyufa husika zisipodhibitiwa mapema huweza hata kusababisha nyumba kubomoka au hata kuanguka.. Nyufa hizi zina madhara ya moja kwa moja kiroho nyufa hizi huleta nyufa kwenye familia, mikosi na hata vifo wakati mizizi ikileta nyufa kwenye nyumba jengo, nguvu yake huleta nyufa katika familia.

Nyufa ndani ya familia husababisha mshikamano uliopo kukatika vipande vipande, watu kukosa ajira, biashara kuanguka, watoto kufeli masomo na vifo hasa vya wazazi
Inasemekana Sio mti mzuri wa kupanda nyumbani na wengi sasa wanaukata Kama unao nyumbani kwako hebu linganisha na hiki nilichoandika hapa.

Je Nini Maoni Yako, Kuna Ukweli Wowote Kuhusu hii?

Maoni yako Tafadhari! Ili Watu Wengine waweze Kupata Uhakika.

SIKILIZA MOJA KWA MOJA USHUHUDA KUTOKA KWA HUYU MTUMISHI